Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yaua watatu wanaodaiwa kuwa majambazi

Mauaji Polisi Dar Polisi yaua watatu wanaodaiwa kuwa majambazi

Thu, 27 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limewaua watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi waliokuwa katika mpango wa kupora katika duka moja la miamala ya fedha eneo la Mbagala Zakhiem jijini Das res Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 27, 2022 Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Jummanne Muliro amesema kuwa tukio hilo lilitokea jana na watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walikuwa wakitumia usafiri wa  pikipiki na baada ya kugundua kuwa wanafuatiliwa na polisi walianza kurusha risasi.

"Baada ya kuanza kurusha Polisi walijihami kwa kutumia silaha ambapo waliwajeruhi na baada ya kufikishwa hospitali waligundua kuwa wameshapoteza maisha, Uchunguzi wa kubaini mtandao wao bado unaendelea," amesema Muliro.

Amesema baada ya ukaguzi walibaini kuwa watu hao walikuwa na bastola moja yenye risasi 11 na fedha bandia Sh1.18 milioni ambazo huzitumia kama geresha kuwa wanataka kuweka fedha kisha kumvamia wakala kwa kumtolea bastola.

"Hiyo bastola ina uwezo wa kutunza rasasi 25 ila tulikuta 11 maana yake 14 zilituma na risasi 14 kwa maisha ya watu ni nyingi sana," amesema Muliro.

Muliro amesema si dhamira ya Jeshi la Polisi kuwaua wahalifu lakini nao hawako tayari kupoteza askari wao hata mmoja hivyo ni lazima wajihami kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live