Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yatangaza dau la milioni 2 kwa atakaye fichua uhalifu

JUMANNE MULIRO Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Jumanne Muliro

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Jumanne Muliro amesema vita dhidi ya Wahalifu Kanda Maalum ya Dar es salaam bado inaendelea na kuwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani nchini.

Amefafanua kwa kusemakuwa Jeshi la Polisi limedhamiria kukomesha vitendo vyote vya uhalifu pamoja na ugaidi, na kuwa limeaanda kiasi cha Shilingi milioni mbili kwa kila mtu atakaye toa taarifa ya matukio ya uhalifu.

"Zawadi bado zinatolewa kwa Mtu yoyote mwenye taarifa za kweli za Majambazi au Wahalifu wanaofanya unyang'anyi wa silaha na taarifa hizo ziwezeshe kukamatwa kwa Mhalifu huyo akiwa na silaha, Polisi itatoa Tsh. Milioni mbili palepale kwa mtoa taarifa kwa siri na hatutomtangaza" Kamanda Jumanne Muliro

Ameongeza kusema kuwa kilichofanyika August 28, 2021 (mauaji ya Hamza) ni chachu ya kuendeleza mapambano dhidi ya Wahalifu huku akisema bado wanaendelea kutoa Milioni mbili kwa kila atakayewezesha kupatikana kwa Wahalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live