Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yataja chanzo mauaji mtumishi wa kanisa Makambako

Jeshi Pic Data Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah

Sun, 13 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Njombe limeeleza sababu zilizotolewa na mtuhumiwa wa mauaji ya mtumishi wa kanisa katoliki lililopo mjini Makambako, Nickson Myamba (48) kuwa ni wasiwasi wa kuchukuliwa nafasi yake katika

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Februari 13, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Daniel Mwilango ambaye alikuwa mtumishi katika kanisa hilo.

Amesema siku ya mauaji hayo yaliyotokea Februari 8 mwaka huu mtuhumiwa huyo aliwasiliana na marehemu kisha kuelekea maeneo ya duka hilo la kanisa kwa ajili ya makabidhiano.

Amesema cha ajabu baada ya kufika dukani hapo kulitokea sintofahamu ambayo ilionyesha kuwa mtuhumiwa huyo alijiandaa kumfanyia uhalifu marehemu.

Kamanda Issah amesema mtuhumiwa huyo alitumia chuma kizito na kumpiga marehemu eneo la kisogoni kisha kumsababishia kupoteza fahamu.

"Alimuongezea chuma kingine yaani pigo la pili na kusababisha marehemu kufariki" alisema Issah.

Ameeleza kuwa baada ya kufariki dunia mtuhumiwa huyo aliamua kutumia panga ili kuutenganisha mwili wa marehemu ambapo kichwa na kifua vilikuwa sehemu yake na kiuno na miguu kilikuwa sehemu nyingine.

Amesema mtuhumiwa huyo alichukua kichwa na kifua na kukihifadhi kwenye mfuko aina ya salfeti huku kiuno na miguu vikiwekwa kwenye boksi.

Amesema baada ya kukamilisha zoezi hilo mtuhumiwa huyo alifunga mlango wa duka kisha akawa anatafuta mbinu ya kuutoa mwili huo harakati ambazo hazikufanikiwa.

"Matokeo yake mtuhumiwa alifunga duka husika na kwenda nyumbani kwake na alichokifanya huko ni kuaga na kuondoka" alisema Issah.

Kamanda Issah amesema Jeshi hilo baada ya kupata taarifa lilifika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu ukiwa kwenye mfuko wa salfeti na mwingine ukiwa kwenye boksi.

Ameeleza kuwa baada ya Jeshi hilo kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa na kumkosa walifanikiwa kukuta suruali yake aliyofanyia tukio hilo ikiwa imetapakaa damu.

Amebainisha kuwa kilichofanyika na Jeshi hilo baada ya kumkosa mtuhumiwa wa mauaji lilianza kumfuatilia na hatimaye kumkamata eneo la Doma wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa anaelekea mkoani Njombe.

Kamanda huyo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa na simu ya marehemu pamoja na funguo mbalimbali Ikiwemo ya chumba ambacho uhalifu ulitokea.

Amesema katika mahojiano mtuhumiwa aliweza kumtaja aliyeshirikiana nae katika mauaji hayo ambaye ni Nickson Valentino mlinzi katika kanisa hilo naye anashikiliwa na jeshi hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live