Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yanasa watuhumiwa 101 wa wizi Morogoro

Kamanda 780x470 Polisi yanasa watuhumiwa 101 wa wizi Morogoro

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro, linawashikilia watu 101 kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali, yakiwemo wizi wa simu na mikoba ya wanawake, wakitumia pikipiki na bajaji ( Vishandu), uvunjaji, upokeaji na ununuzi wa mali za wizi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Fortunatus Musilimu, amesema hayo leo kwa waandishi wa habari, kuhusu operesheni kali inayoendelea ya kupambana na uhalifu, ambayo ilianza Septemba 12, mwaka huu .

Musilimu amesema katika oparesheni hiyo watu 101 walikamatwa kwa tuhuma za makosa mbalimbali, ikiwemo kukamatwa pikipiki 10 za aina mbalimbali zisizo na namba za usajili, zinazosadikika zikitumiwa na baadhi yao kufanikisha uhalifu huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live