Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yanasa 21 mtandao wizi wa ng’ombe Pwani

Ngombe Kiofo Hai Polisi yanasa 21 mtandao wizi wa ng’ombe Pwani

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani llinawashikilia watu 21 kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Agosti 19, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia msako wa jeshi hilo iliyofanyika usiku na mchana baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo Julai 27 mwaka huu.

"Mnao tarehe 27 mwezi wa 7 mwaka huu saa saba usiku huko Mkenge, Kata ya Kiwangwa mkoani wa Pwani mtu mmoja jina tunalihifadhi kwa sasa, aliibiwa ng'ombe wake nane baada ya kuvunjiwa zizi na watu ambao hawakujulikana tulipopata taarifa hiyo tulifanya msako na kuwakata watuhumiwa hao," alisema.

Lutumo alisema kuwa katika tukio hilo Vijana wawili waliokuwa wakikaa kwenye zizi hilo kwa ajili ya malisho na ulinzi mmoja wao anadaiwa kuuwawa na watuhumiwa hao na mwingine kujeruhiwa.

"Mmoja Kati ya vijana hao waliokuwa wamekabidhiwa kulinda Kambi hiyo ya mifugo, Hamis Hassan mkazi wa Mkenge alifanikiwa  kuwatoroka watuhumiwa hao huku mwenzake Ally Msonde mkazi wa Mkenge hakuwatoroka na badaye alikutwa akiwa amefariki umbali wa mita 200 kutoka kwenye eneo hilo," alisema.

Alisema kuwa baada ya kukamatwa watuhumiwa hao Agosti 17 mwaka huu maeneo ya Masuguru Kata ya Kiwangwa Wilayani Bagamoyo mtuhumiwa mmoja kati yao aliyefahamika kwa jina la Idd Charles Mkazi wa Mkenge alijeruhuwa na lisali na Jeshi la Polisi mguuni tukio lililosababisha kuvuja damu nyingi ambapo alifariki wakati akiwa njiani kupelekwa Hospitali.

Alisema kuwa watuhumiwa hao watafishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazowakabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live