eshi Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Haji Musa (30)mkazi wa Chamazi kwa tuhuma za kumshambulia kwa fimbo na kumjeruhi mtoto wake wa kambo wenye umri wa miaka 11, ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP), Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea usiku wa Februari 22, 2022 katika eneo la Chamazi wilaya Temeke.
ACP Muliro amesema siku hiyo ya tukio, Mussa alimtuhumu mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Chamazi Dovya kuwa amemuibia Sh195,000.
" Baada ya kumtuhumu kuwa mtoto huyo wa kambo amemuibia Sh195,000 mtuhumiwa( Mussa) alimshambulia kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali" amesema Kamanda Muliro.
Kamanda huyo amesema kuwa Februari 23, 2022 mtoto huyo alienda shuleni na ilipofika saa 6:30 mchana alianguka na kumpoteza fahamu, ambapo alinyanyuliwa na kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
" Uchunguzi wa awali inaonyesha kuwa chanzo cha mtoto huyo kuumwa ni kipigo alichokipata kutoka kwa baba yake wa kambo" amesema Muliro na kuongeza.
"kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa ni cha ukatili uliopitiliza na jeshi ya Polisi haliwezi kuvumilia vitendo hivi" amesema Murilo.