Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yamshikilia mwanamke kwa unyanyasaji wa mtoto

Ugandan Woman 1024x696 Polisi yamshikilia mwanamke kwa unyanyasaji wa mtoto

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Uganda, linamshikilia Dorothy Nabulime (22) mkazi wa mji mdogo wa Busula, nje kidogo ya jiji la Kampala kwa tuhuma za kumpiga na kumfanyia ukatili mwanae wa kike mwenye umri wa miaka miwili.

Dorothy mama wa watoto watatu alirekodiwa video akimpiga mwanae huyo bila huruma na kumuangusha kwenye beseni alilokua anaogea.

Mwanae mkubwa ana miaka 5 ambaye alimzaa akiwa na miaka 17. Wa pili ana umri wa mitatu na wa mwisho ana miaka miwili ambaye ndiye aliyerekodiwa akimpiga.

Dorothy ni “single mother” ambaye anadaiwa kupitia unyanyasaji wa kijinsia katika malezi yake, na anawalea watoto wote watatu peke yake kwa biashara ndogondogo.

Amefunguliwa kesi ya shambulio la kudhuru mwili (assault causing bodily harm) na unyanyasaji wa mtoto (child abuse) na anatarajiwa kupandishwa kizimbani kesho, jumatatu kujibu tuhuma zinazomkabili. Kwa sasa anashikiliwa kituo cha polisi Luwero, huko Busula na amefunguliwa kesi nambari SD/RF/06/03/09/2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live