Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakamata watu 59 wakiwa na dawa za kulevya

Polisi Pc 660x400.jpeg Polisi yakamata watu 59 wakiwa na dawa za kulevya

Mon, 3 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Watu 59 wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ya jinai, ikiwemo kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroin gramu 1.25, mirungi kilo 456, misokoto 1,401 ya bangi na bastola moja iliyokuwa ikimilikiwa kinyume cha sheria.

Akiongea na Waandishi wa habari Kituo cha Polisi Himo, RPC wa Kilimanjaro, Amon Kakwale amesema watu hao  walikamatwa katika operesheni na misako iliyoendeshwa na jeshi hilo kuanzia April 16 hadi Mei mosi 2021.

Amesema mbali na Dawa za kulevya, pia wamekamata vyombo vya usafiri ambavyo ni magari nne na pikipiki tano, vilivyokuwa vikisafirisha mirungi na gari moja iliyokuwa ikisafirisha simu za magendo na kwamba vyombo hivyo vitataifishwa kwa mujibu wa sheria.

“Pia tumekamatwa Pombe haramu aina ya Gongo lita 223, mitambo 4, ya kutengeneza gongo, nyavu haramu za uvuvi (makokoro) 180 pamoja na simu za kiganjani 237 za aina mbalimbali, zilizoingizwa nchini kwa njia za magendo,” RPC Kilimanjaro

“RAIS SAMIA WATU WANAKUFA BILA HATIA” OBASANJO AKIONGEA IKULU ATOA POLE KIFO HAYATI MAGUFULI, MKAPA

Chanzo: millardayo.com