Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakamata wahamiji haramu wakibadili fedha

8283e46b11bff3e68d66a55a95da1849 Polisi yakamata wahamiji haramu wakibadili fedha

Sun, 22 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAHAMIAJI haramu 12 wamekamatwa katika eneo la Mbande Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakiwa njiani kuelekea Afrika Kusini kupitia Zambia .

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema, wahamiaji hao walikamatwa wakati wakibadilisha fedha kutoka dola kwenda shilingi.

Tukio la kukamatwa kwa wahamiaji haramu mkoani Dodoma ni la pili ndani ya wiki moja baada ya wengine 29 kukamatwa katika eneo la Mtera, wilayani Mpwapwa wakielekea Makambako kwa lengo la kuvuka mpaka ili kwenda Afrika Kusini.

Muroto alisema, katika kundi hilo la wahamiaji haramu waliokamatwa Mbande, Waethiopia ni 11 na mmoja ni Mkenya. Walikuwa wakibadilisha fedha kupata fedha za Tanzania ili kuvuka mpaka wakiwa pamoja na Mtanzania ambaye aliwatelekeza katika duka hilo.

Muruto alisema wanahojiwa na Jeshi la Uhamiaji na mahojiano yakikamilika watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo za kuingia nchini kinyume cha sheria .

Kamanda Muroto aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi kwa kutoa taarifa mara wanapoona watu ambao hawajulikani vizuri katika maeneo yao.

Chanzo: habarileo.co.tz