Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakamata vijana 17 wanaojiita ‘Ibilisi’

Ibilisipic Kamanda wa Polisi Mkoani Mkoa Tanga , Safia Jongo

Sat, 6 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Jeshi la Polisi Mkoa Tanga Oktoba 2021 limewakamata watoto 17 wanaojiita ‘ibilisi’ katika oparesheni iliyofanyika mkoani humo kwa tuhuma za kufanya uhalifu.

Akitoa taarifa leo Jumamosi Novemba 6, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Safia Jongo amesema ameuwasha moto wa kupambana na watoto hao wa ‘ibilisi’ ambao wamekuwa tishio kwa wakazi wa mkoa huo.

"Nimetoka Tabora kulikua na watoto wanajiita Roho Saba, nimekuja Tanga nimekuta watoto wanajiita Ibirisi tena wanamiaka 12 hadi 18, nilipambana na watoto wa roho saba mpaka nikawamaliza, sasa nitapambana na watoto hawa wa ibilisi .

“ Mtoto wa ibirisi na wazazi wake pia ni ibilisi hivyo nitapambana na wazazi wao pia na tumeshawakamata wazazi wanne na tunatarajia kuwafikisha mahakamani uchunguzi utakapokamilika” amesema Kamanda Safia.

Kamanda Jongo amesema baadhi ya watoto hao wamekabidhiwa kwa wazazi wao kulingana na umri wao na wengine wamefikishwa mahakamani .

Baadhi ya wakazi wa Tanga wamelipongeza Jeshi hilo kwa kufanya msako wa kuwakamata watoto hao ambao ni tishio kwa wakazi wa mjii huo.

Chanzo: mwananchidigital