Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakamata shehena ya madawa ya kulevya

Madawa Arusha Polisi yakamata shehena ya madawa ya kulevya

Sat, 5 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumkamata kilo 187 za dawa za kulevya aina ya Mirungi zikisafirishwa na ELIA MBWAMBO (45) mkazi wa Ngaramtoni

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP JUSTINE MASEJO amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa leo Machi mosi saa sita na nusu mchana katika eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha na askari wa doria,akiwa na gari lenye namba za usajili T.793 CUY aina Varian.

Amesema kuwa Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu ya usafirishaji wa dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali jijini Arusha.

Na kusema kuwa mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya kulitolea maamuzi kisheria.

ACP Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili kutokomeza kabisa uhalifu ndani ya mkoa huo pamoja na kuwataka wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya dawa hizo haramu kuacha mara moja tabia hiyo kwani hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live