Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakamata magari 1527 msako usalama barabarani

Vingora Taa Polisi yakamata magari 1527

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbrod Mutafungwa amesema Polisi kimefanikiwa kuyakamata magari 1527 yakiwa na vimulimuli au ving'ora kinyume cha sheria na kanuni za usalama Barabarani ambapo mkamato huu unajumuisha magari madogo na malori.

"Idadi ya pikipiki na bajaji zilizokamatwa zikiwa na vimulimuli na ving'ora visivyo rasmi ni 1358, idadi ya magari ya Watu binafsi na ya Serikali yaliyokamatwa yakitumia namba bandia ni 73"

"Tunawakumbusha kwamba magari yanayopaswa kuwa na ving'ora na vimulimuli kwa dharura ni magari ya kubeba Wagonjwa (Ambulance), magari ya zimamoto, magari ya vyombo vya ulinzi na usalama na magari mengine ni yale yaliyopatiwa kibali na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali (magari hayo ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa)”

“Kama kuna Mtu yeyote kwa dharura anahitaji kutumia ving'ora anatakiwa kuomba kibali kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi au kwa Jeshi la Polisi iwapo atakubaliwa atasindikizwa kwa kutumia ving'ora na sio vinginevyo" imeeleza taarifa ya Wilbrod Mutafungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live