Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yadaka magari 23 yaliyoibiwa

Maegesho Ya Magari Polisi yadaka magari 23 yaliyoibiwa

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Mohamed Amani (45)maarufu Kiziwi, Mkazi wa Dar es Salaam na Mwanza, pia limemkamata Salome Richard (32) maarufu Mama G Mkazi wa Mwanza na wenzao wanane kwa tuhuma za wizi wa magari katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika operesheni hiyo kali, Jeshi la Polisi limeyakamata magari 23 aina mbalimbali, ambayo ni IST 5, fuso 1, Nissan Civilian 1, Coaster 1, Toyota Hilux pickup 1, Nissan patrol 1, Toyota Premio 2, Probox 1, Spacio 2, Harrier 2, Ravfour 3, Town Hiace 2 na Hiace 1, magari haya yamekamatwa katika Mikoa ya Mwanza, Iringa, Kilimanjaro, Kagera, na Dar es Salaam.

Baada ya kuwahoji kwa kina Watuhumiwa na hivyo kuwapeleka Wapelelezi yalipo magari hayo, upelelezi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa Watuhumiwa hawa kabla ya kuiba huvizia magari hayo yakiwa yameegeshwa kwenye maegesho ya jumla, binafsi na majumbani baadae kuvunja vitasa vya milango ya upande wa dereva na kuwasha gari kwa kutumia fungo bandia na kuondoka.

Aidha Watuhumiwa hao baada ya kuiba magari hayo hubandika namba za usajili na chasses za magari yaliyopata ajali na kuuzwa kama vyuma chakavu na makampuni ya bima baadae kuyauza tena magari hayo waliyoyaiba, baadji ya magari yameshatambuliwa na Wamiliki na upelelezi unaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live