Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yadaka 26 wakidaiwa kufanya uharifu Tanga

MBARONI.jpeg Polisi yadaka 26 wakidaiwa kufanya uharifu Tanga

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

eshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 26 walioingia kwenye Hoteli ya Mambo View, iliyopo katika Kijiji cha Mambo, Kata ya Sunga Tarafa ya Mtae, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga na kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma za uhalifu zinazowakabili.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Leo, Novemba 09, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime imesema watuhumiwa hao walidaiwa kufanya uhalifu huo Oktoba 23, mwaka huu.

Mbali na tukio hilo, taarifa hiyo, Misime amesema watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma zingine za kufanya unyang’anyi wa kutumia nguvu na shambulio la kudhuru mwili wa ‘Dagmara Anna Ikiert’.

“Watuhumiwa hao 26, walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Oktoba 26, 2023 kujibu tuhuma hizo kwa mujibu wa sheria,”amesema

Misime amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na taasisi nyingine wanaendelea kukamilisha ukusanyaji wa ushahidi ambao unahitaji chunguzi zaidi ili kesi hiyo iweze kwenda katika hatua inayotakiwa.

“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mwenye ushahidi mwingine wa ukweli asisite kuufikisha polisi ili uweze kufanyiwa kazi,” amesema.

Misime amesema jeshi hilo halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote yule atakayebainika kuhusika kwa namna yeyote ile au kwa kupanga, kuhamasisha, kutoa taarifa za uongo au kufadhili,“ amesema Misime

Chanzo: www.tanzaniaweb.live