Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wazungumzia jinsi wanafunzi walivyobakwa

65432 Pic+ubakaji

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rombo. Wanafunzi wiwili wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Kilamfua wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro  wamebakwa na mwanaume mmoja wakiwa katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro wakiokota kuni.

Akizungumza leo Jumatano Julai 3, 2019 kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea jana Julai 2, 2019.

Amesema kwa mujibu wa wanafunzi  hao wenye umri wa miaka 15,  wakati wakiendekea kuokota kuni alitokea mtu huyo ambaye hawakumtambua na kuanza kuwafanyia kitendo hicho cha kikatili.

Issah amesema  wanafunzi hao wanaopatiwa matibabu katika  Hospitali ya Huruma wamedai mtu huyo alianza kumbaka mmoja baada ya mwingine.

Chanzo: mwananchi.co.tz