Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waua watu watatu Mwanza

40419 Mwanzapic Polisi waua watu watatu Mwanza

Thu, 7 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza.  Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limewaua watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia leo Jumatano Februari 6, 2019.

Tukio hilo ni la pili kwani Januari 25, 2019 polisi waliwaua watu wanane waliodaiwa kuwa ni majambazi wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kaimu kamanda wa polisi mkoani humo, Advera Bulimba amesema tukio hilo limetokea Mtaa wa Nyakabungo, kata ya Isamilo saa 8 usiku wakati watu hao wakijaribu kufanya uhalifu wa kuvunja maduka.

Amesema majambazi hao walikuwa na silaha ya moto ambayo haijafahamika ni ya aina gani.

Amesema kulingana na taarifa walizopata kutoka kwa wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo, majambazi hao walikuwa   takribani sita lakini wengine walifanikiwa kukimbia.

"Tulipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna watu wanavunja maduka na kupiga risasi hewani, hivyo askari waliokuwa doria walifika haraka eneo la tukio na walifanikisha kuwaua hao wawili na wengine wakakimbia. Hawakufanikiwa kuiba chochote,” amesema.

"Tumekamata silaha mbalimbali za jadi yakiwemo mapanga, nondo na mikasi. Bado kikosi kazi kipo eneo la tukio kufanya uchunguzi zaidi. Na miili imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa Sekou Toure," amessema Bulimba.

Mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Asela Peter amesema watu hao walianza kupiga risasi hewani wakitishia watu wasitoke nje na kuanza kukata kufuli lakini waliwahiwa kabla ya kufanya uhalifu wowote.

Soma Zaidi: Baba aeleza alivyoshuhudia mwanaye akipigwa risasi kanisani



Chanzo: mwananchi.co.tz