Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waua watatu kwa risasi

11549 MAUAJI+PIC TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma.  Jeshi la polisi mkoani Kigoma limewaua watu watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi huku wanne wakifanikiwa kukimbia.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 12, 2018 kamanda wa polisi mkoani humo, Martin Ottieno amesema tukio hilo limetokea juzi Agosti juzi 10, 2018 saa  5:30 usiku katika kijiji cha Kigina wilayani Kibondo mkoani hapa.

Amesema katika tukio hilo polisi walikamata risasi 69, bunduki aina ya AK 47 yenye usajili wa nchi jirani ya Burundi na magazine tatu.

Amesema watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi walimuua  mkazi wa eneo hilo,  Lukas Luchapa (38)  aliyekuwa akitokea matembezini.

Amesema wakati wakipanga magogo barabarani kuzuia magari, alitokea mtu huyo na walimshambulia  kwa risasi.

“Tulipata taarifa hizo na kwa kushirikiana na wananchi tulifuatilia na kubaini walikuwa saba,” amesema Kamanda Ottieno.

Amebainisha kuwa katika msako walioufanya walikutana na watu hao katika msitu uliopo karibu na kijiji hicho na kuanza kupambana nao.

Amesema polisi walifanikiwa kuwaua watatu huku wanne wakitokomea kusikojulikana

“Niwaombe wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi kwa kutoa taarifa watakapomuona mtu mgeni na kumtilia mashaka,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz