Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waua wanne mkoani Kigoma

85060 Wauwa+pic Polisi waua wanne mkoani Kigoma

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kasulu. Jeshi la polisi mkoani Kigoma limewaua watu wanne wanaodaiwa kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uhalifu katika nyumba aliyofikia mfanyabiashara wa ng’ombe.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2019 kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amesema tukio hilo lilitokea  jana alasiri eneo la Mvugwe wilayani Kasulu na kwamba wengine watatu walitoroka.

Amesema baada ya polisi kupata taarifa za watu hao waliotaka kumvamia mfanyabiashara huyo aliyechukua fedha Kasulu walijipanga na kufika eneo la tukio, “tulikamata bunduki moja aina ya AK 47, risasi 48, panga, shoka pamoja na rungu. Walishtuka baada ya kuona askari na walianza kuwarushia risasi askari.”

Wakati huohuo, polisi mkoani humo linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji , Zakaria Richard (30) kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tano wa shule hiyo.

Mwalimu huyo alikuwa akimfundisha masomo ya ziada mwanafunzi huyo baada ya kuombwa na wazazi wake.

Amesema siku ambazo mwanafunzi huyo alishindwa kwenda katika masomo hayo, Richard alikuwa mkali jambo lililowapa wasiwasi wazazi wake na walipofuatilia walibaini  mtoto wao anafanyiwa vitendo hivyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz