Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waua panya road wawili Dar

Jumanne Muliro Dsm Polisi waua panya road wawili Dar

Sun, 31 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwapiga risasi zilizopelekea vifo vyao Vijana wawili Bakari Ismail (21) na Shomari Kacheuka maarufu Babuu (22) Wakazi wa Vingunguti Jijini Dar es salaam ambapo wamesema Vijana hao walikuwa Wahalifu (Panya Road) na kwamba mwenzao wa tatu bado mwili wake upo Amana Hospital na wenzao wengine wamekimbia.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema “December 27,2023 lilipokea taarifa kutoka kwa Wananchi wanaochukia uhalifu meneo ya Vingunguti kuwa kuna kundi la Watu vijana akiwemo Panya White kama kiongozi wao wanajiandaa kukufanya matukio ya kihalifu maeneo ya Vingunguti ambapo ufuatiliaji ulianza na Polisi walipofika maeneo ya Vingunguti darajani majira ya saa 2:00 usiku waliwakuta Watu sita wakiwa na silaha za jadi (mapanga) wakiwa wamekusanyika”

“Polisi waliwataka wajisalimishe ili wakamatwe, kinyume chake wakataka kuwashambulia Polisi kwa mapanga, Polisi walijihami na kufyatua risasi hewani lakini mazingira yalivyozidi kuwa ya hatari zaidi Polisi walilazimika kuwajeruhi kwa risasi miguuni na hapo watatu miongoni mwao walifanikiwa kukamatwa huku wakiwa na mapanga matatu yaliyopatikana eneo hilo la tukio”

“Polisi waligundua baadaye kuwa waliokuwa wamejeruhiwa eneo hilo ni pamoja na Paka Pori maarufu Shommy ambaye baadae alijulikana kwa jina la Shomari Salehe Kucheuka na Beka aliyejulikana baadaye kama Bakari Athumani, waliokimbia ni Panya White na mwingine ambaye hajafahamika, hao waliokamatwa baada ya kujeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu lakini baada ya kufikishwa pale Madaktari walibaini kuwa tayari walikuwa wamepoteza maisha”

“Maiti mbili za Shomy na Beka tayari zimetambuliwa na Ndugu zao na maiti moja ya Paka Pori bado ipo Hospitali ya Amana haijatambuliwa na Ndugu na upelelezi wa tukio hili na matukio mengine ya eneo hilo unaendelea”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live