Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watuhumiwa kushika nyeti za wanawake kinguvu

Dc NCHEMBE Mkuu wa wilaya ya Handeni, Seril Mchembe

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: muungwana Blog

Wanawake kutoka wilaya ya Handeni mkoani tanga wamelalamikia baadhi ya vitendo vinavyofanywa na Askari wa jeshi la polisi kuwatomasa na kuwata kingono kwa lazima.

Wanawake hao wamepaza sauti zao baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya Askari wa jeshi la polisi mbele ya mkuu wa wilaya ya Handeni Siriel Mchembe kwenye mkutano wa kamati ya ulinzi na usalama.

Akielezea shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa kuna Askari wakienda wanawashika bila ridhaa yao na kuwataka kilazima na ukikataa wanakutafutia sababu na kukukamata kwenda kukulaza lock up.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Seril Mchembe amesema kuwa hakuna Askari mwenye mamlaka ya kumgusa mwanamke au kumcheze kwenye maeneo yake bila kibali chake kwani cheo cha mtu hakihusiani na mwili wa mtu.

Chanzo: muungwana Blog