Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watoa tamko Polepole kuvunjiwa nyumba

Pole Pole Polisi watoa tamko Polepole kuvunjiwa nyumba

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, limetoa tamko juu uvamizi uliofanyika nyumbani kwa Mbunge wa Kuteuliwa Humphrey Polepole katika mtaa wa Mabuba jijini humo na kusema kuwa wanaendelea na msako mkali ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo.

Polepole aliripoti kutokea kwa tukio hilo jana Desemba 12, 2021 na kubaini kuvunjiwa dirisha la nyumba anayoishi, kuibiwa TV moja ya Inch 55 pamoja na spika moja ya Bluetooth huku wakiacha mazingira ya nyumba yote yakiwa katika mpangilio usio rasmi.

"Jana tarehe 12/12/2021 majira ya saa tatu na nusu katika mtaa wa Mabuba jijini Dodoma mbunge Humphrey Polepole alibaini kuvunjiwa dirisha la nyumba anayoishi na kuibiwa flat screen TV moja inch 55 na Specker moja ya Bluetooth, thamani ya mali yote hiyo bado haijaweza kufahamika"

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mbunge Humphrey Polepole umebaini alisafiri kwenda mkoa wa Manyara katika shughuli zake, upelelezi wenye kuambatana na msako mkali unaendelea ili kuwatafuta wahusika wa tukio hilo na kuwachukulia hatua za kisheria" Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), OnesmoLyanga.

Kuhusu yanaoendelea mtandaoni juu ya tukio hilo kuunganishwa na mambo ya kisiasa yaani kuchukuliwa kama vita ya kisiasa kwa kurejelea kauli aliyotoa mbunge huyo kuhusu watu aliowaita 'wahuni', Jeshi la Polisi limesema halioni kama sula hilo lipo kisiasa.

"Suala la kwamba ni habari ya siasa sisi hatuoni kwa sababu makazi yamevunjwa kwa hiyo huwezi kusema wahalifu walikuwa wanamtafuta yeye, wangemkuta mwenyewe ishu ingekuwa tofauti ingekuwa ni unyang'anyi wa kutumia silaha au nguvu, bado haieleweki ni lini hasa palivunjwa kwa hiyo si rahisi kujua kulikuwa na nia ya kutaka kumdhuru yeye kama yeye kwa sababu hakuna ujumbe wowote ambao tumeweza kubaini kuwa umemtishia yeye maisha yake"- Amesisitiza Kamanda huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live