Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wathibitisha mdogo wake Heche kuuawa na Polisi kwa kisu

7165 IMG 4550.jpeg TZW

Sun, 29 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kuuawa kwa, Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche kwa kuchomwa kisu na polisi.



Kamanda Mwaibambe amekiambia EATV kuwa, marehemu alikuwa na mgogoro na mmoja ya askari waliokuwa wamemkamata, na kufikia hatua ya kutaka kushikana (kupigana) ndipo askari aliposhindwa kujizuia na kumchoma kisu.

“Tukio ni la kweli limetokea na huyo askari tunamshikilia, huyo kijana alikamatwa usiku sasa wakati wapo kwenye gari wakielekea kituo cha polisi, ukatokea mzozo kati ya huyu askari na huyu marehemu, mzozo kama wanataka kupigana, mwenzake akaingilia kuamua, lakini ni kweli askari amemjeruhi huyu mgongoni,”amesema Kamanda Mwaibambe

Aidha, Sambamba na hilo Kamanda Mwaibambe amesema hali ya kituoni hapo kwa sasa imetulia baada ya wananchi kufurika kulalamikia mauaji hayo, na kwamba amezungumza na ndugu wa familia kuwaeleza jinsi tukio lilivyokuwa.

Hata hivyo, Kamanda Mwaibambe amewataka watu kutochukulia tukio hilo kisiasa, isipokuwa ni kama tukio lingine la mauaji, ingawa sio jambo zuri kwa mtu yeyote

Chanzo: bongo5.com