Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watatu mbaroni tuhuma unyang'anyi wa Sh90 milioni

HUKUMU Polisi watatu mbaroni tuhuma unyang'anyi wa Sh90 milioni

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa watatu wa Jeshi la Polisi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wakikabiliwa na shtaka moja la unyang'anyi wa kutumia silaha na kujipatia Sh90 milioni kutoka kwa Grace Matage.

Askari hao ni mwenye namba F 7149 D/ Coplo Ramadhani (42) maarufu kama ‘Rasta’ na mkazi wa Kipawa. Mwingine ni G. 7513 D/ Coplo Majid Abdallah (35) mkazi wa Kunduchi na WP 6582 D/ Coplo Stela Mashaka.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Jumanne Oktoba 31, 2023 na kusomewa shtaka moja la unyang'anyi wa kutumia silaha na wakili wa Serikali Neema Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amir Msumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live