Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watangaza operesheni nyakuanyakua kwa bodaboda

36801 BodabodapicPolisi watangaza operesheni nyakuanyakua kwa bodaboda

Thu, 17 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Polisi wa usalama barabara wamesema mwaka 2019 ni mwaka wa nyakuanyakua kwa waendesha bodaboda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu Januari 14, 2019 Jijini Dodoma, kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Fortunatus Muslim alisema nyakuanyakua  inahamia kwa waendesha bodaboda baada ya kuonyesha mafanikio makubwa kwa wenye magari.

Muslim alisema jeshi hilo halitakuwa na mjadala kwa wote wanaovunja sheria za usalama barabarani ikiwemo wanaoendesha bodaboda bila ya kuvaa kofia ngumu (helmet)

Alisema ziko mbinu ambazo polisi wa barabarani watapewa ili kuepuka madhara wakati wa ukamataji lakini ikibidi kutumia nguvu watafanya hivyo ili mradi iwe kwa nia ya kuzuia au kupunguza ajali za barabarani.

Muslim alisema huu si muda wa kucheka na madereva wazembe kwani wanaendelea kulitia hasara taifa na kupoteza nguvu kazi ambayo ingekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi.

“Nitoe rai kwa bodaboda wote wanaovunja sheria kwamba nyakuanyakua hii haitawaacha salama, wanabebana mishikaki lakini wakipata ajali Serikali inatumia gharama kubwa kuwatibu, hatutakubali sasa,” alisema Muslim.

Akifunga semina ya siku moja kwa wajumbe wa mabaraza ya usalama barabara nchini, Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Yusufu Masauni aliagiza polisi kuwa wakali wakati wote kwani ukali ndio ambao unasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Masauni alimuagiza kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kuwasimamia vema askari wake na kuwawajibisha wale watakaokwenda kinyume cha maadili ya kazi zao.



Chanzo: mwananchi.co.tz