Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wasimamishwa kwa kumpiga raia

Arkansas .png Polisi wasimamishwa kwa kumpiga raia

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi watatu katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wamesimamishwa kazi kutokana na video iliyozaagaa mitandaoni ikiwaonesha wakimpiga mshukiwa mmoja huku wamemlaza chini.

Mmoja wa maofisa ameonekana akimpiga mtu huyo kichwani mara nyingi huku akimpigiza kichwa kwenye sakafu. Ofisa mwingine wa polisi ameonekana amepiga magoti huku anampiga mshukiwa huyo.

Mtu huyo baada ya kupigwa alionekana akijikinga kichwa chake kwa mikono yake huku akijibiringisha barabarani kujilinda. Video hiyo imetazamwa na mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kuzua minongóno.

Mtu huyo aliyekamatwa alikua na tuhuma za kusababisha vitisho kwenye duka moja, ambapo polisi walipigiwa simu kuja kumkamata alijihami kwa kumsukuma askari mmoja aliyeanguka chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live