Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi washukuru wananchi, ikikamata silaha 199

D135694ad6f23bd5b569a880bc503eaa Polisi washukuru wananchi, ikikamata silaha 199

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi nchini limewashukuru wananchi wote kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa mwaka uliopita wa 2020 na kusema kupitia ushirikiano huo walifanikiwa kuzuia uhalifu na kukamata silaha na vitu vingine haramu zikiwemo aina mbalimbali za silaha 199 na risadi 360.

Miongoni mwa silaha hizo ni AK 47, 10 bastola 16,Shotgun 39 na magobore 134 na jumla ya watuhumiwa 177 waliokamatwa kati yao ni wananume 170 na wanawake ni saba.

Aidha, kupitia ushirikiano huo mzuri kwa jeshi hilo, Polisi ilifanikiwa pia kukamata dawa za kulevya kilogramu 25,110.102 za dawa tofauti ikiwemo cocaine , heroin na bangi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana mjini Dodoma na Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ya kuwashukuru wananchi kwa kulipa jeshi hilo ushirikiano mzuri ushirikiano huo umewezesha nchi kuendelea kuwa salama kipindi chote cha mwaka 2020.

Alisema watuhumiwa hao waliokamatwa walikuwa wakitumia silaha hizo katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha,mauaji,uwindaji haramu na kumiliki silaha isivyo halali.

Kuhusu dawa za kulevya, Kamanda Misime alisema jumla ya kilogramu 25,110.102 zilikamatwa za aina tofauti ikiwemo kilo 13,230.22 za bhangi, kilo 11,804.864 za mirungi, kilo 4.52 za kokeni na kilo 70.5 za heroin.

Alisema watuhumiwa 9,265 wa dawa hizo wamekamatwa na kesi zao zipo mahakamani kwenye hatua mbalimbali.

Aidha alisema kwa mwaka 2020, polisi pia walikamata pombe haramu ya gongo lita 69,295.30 na mitambo 379 ya kutengeneza pombe hiyo na watuhumiwa wake ni 7,169 na mashitaka yao yako mahakamani katika hatua mbalimbali.

Akizungumzia uhalifu kupitia mitandao ya simu kwa mwaka 2020, Kamanda Misime alisema jumla ya makosa 4,850 yaliripotiwa na watuhumiwa 634 walikamatwa wakiwemo wanaume 490 na wanawake 144.

“Katika makosa ya uhalifu kupitia mitandao ya simu mwaka 2020 yaliripotiwa makosa, 4,850 na wahalifu 634 wamekamatwa na baadhi ya wahalifu hao wametenda uhalifu huo zaidi ya mara moja,” alisema Kamanda Misime.

Akizungumzia mwaka 2021, Kamanda Misime alisema umeanza vizuri na kuwa nchi iko salama pamoja na kuwa na matukio machache yaliyojitokeza kuanzia Januari 2021 ambayo yameendelea kushughulikiwa hadi sasa na makamanda wa polisi.

Chanzo: habarileo.co.tz