Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi washangaa Sheikh Gora kutekwa Mwanza

31602 Pic+sheik Sheikh Bashir Gora

Fri, 14 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Jeshi la Polisi limesema linasikitishwa na kushangazwa na tukio la kutekwa kwa Sheikh Bashir Gora ambaye ni mkuu wa chuo cha dini ya Kiislamu cha Nyakato jijini Mwanza.

Chuo hicho (Nyakato Islamic Institute) kipo chini ya taasisi ya The Registered Trustees of Islamic.

Sheikh Gora alitekwa Desemba 6 na watu wasiojulikana baada ya kijana mmoja kwenda nyumbani kwake kuulizia nafasi ya shule kwa ajili ya mdogo wake na baadaye kiongozi huyo alisogea nje kidogo kwa mazungumzo na kijana huyo kabla ya mtu mwingine kujitokeza na kumkamata na kumuingiza kwa nguvu ndani ya gari kisha watekaji kutoweka naye.

Jeshi la Polisi halikuwahi kuzungumzia tukio hilo, lakini jana Kamanda Jonathan Shanna alizungumza.

“Hizi taarifa tumezipokea kwa masikitiko makubwa,” alisema Kamanda Shanna akiongea na Mwananchi.

“Huyu ni kiongozi wa dini, mlezi wa maadili, hakuwa na shida na mtu yeyote. Lakini niwahakikishie familia na jamii waondoe hofu tutampata kwa kutumia mbinu zetu za kipolisi.”

Hata hivyo, Kamanda Shanna alisema bado hawajapata taarifa na vielezo vizuri, hususan usafiri uliotumika kumchukua.

“Hatujafahamu vizuri maana waliokuwapo wakati anachukuliwa walishindwa kujua aina ya gari, namba za gari na uelekeo. Pia hatujafahamu waliomchukua ni kwa sababu ya tofauti za kiimani, kibiashara au kijamii. Lakini yote haya tunayafanyia kazi na tunaomba tushirikiane kupata taarifa zaidi,” alisema.

Mama: Mwanangu hayupo tena

Katika mahojiano na Mwananchi, mdogo wa sheikh huyo anayeitwa Khalili Gora alisema kazi hiyo wanamwachia Mungu na vyombo vya dola.

Alisema tukio hilo limewaumiza kwa sababu ni la kwanza kutokea kwenye familia yao yenye watoto saba yeye akiwa ni watatu kuzaliwa.

Alisema walijaribu kumficha mama yao taarifa za kutoweka kwa Sheikh Gora, lakini alipopata alilia akisema “mwanangu atakuwa hayupo tena”.

Shekh Gora ana wake wawili na watoto saba. “Sisi tunaamini ndugu yetu hana makosa na mtu maana hatujawahi kusikia. Kwa kuwa serikali ina watu na mbinu nyingi, imani yetu wataweza kumpata,” alisema Khalili.

Ilivyokuwa

Kwa mujibu wa Sadik Mchola, katibu wa taasisi inayomiliki chuo, shule ya awali, msingi na sekondari ya Nyakato Islamic,

Kabla ya Sheikh Gora kuchukuliwa, kijana mmoja alimfuata akidai anataka fomu kwa ajili ya mdogo wake kujiunga na chuo hicho.

Baada ya kuambiwa fomu zitatolewa Januari, aliondoka na kurudi mara kadhaa huku kitaka pia fomu kwa ajili yake ya kujiunga na sekondari. Baada ya kupewa fomu hiyo alisindikizwa na Sheikh wakielekea nyuma ya chuo ambapo kulikuwa na gari ndipo alishuka kijana mwingine wakambeba kwa nguvu kumuingiza kwenye gari na kuondoka kwa haraka.

Matukio ya utekaji yalipungua, lakini yakaibuka mwishoni mwa mwaka wakati mfanyabiashara maarufu, Mohamed Dewji alipotekwa na watu wasiojulikana.

na kutelekezwa siku kadhaa baadaye.



Chanzo: mwananchi.co.tz