Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wapinga aliyechana kitabu cha dini kupewa dhamana, apelekwa mahabusu

94972 Pic+kitabu Polisi wapinga aliyechana kitabu cha dini kupewa dhamana, apelekwa mahabusu

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mahakama ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imemnyima dhamana Daniel Maleki aliyefikishwa katika mahakama hiyo jana Ijumaa Februari 7, 2020 baada ya kuchana kitabu cha dini.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Februari 8, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema kutokana na kulinda usalama wa mtuhumiwa huyo wameiomba mahakama kuzuia dhamana ombi ambalo limekubaliwa.

Amesema ombi hilo la kuzua dhamana liliwasilishwa mahakamani hapo na polisi chini ya kifungu namba 148 kifungu kidogo cha 5 (d) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Akieleza tukio hilo, Mutafungwa amesema lilitokea saa 8 mchana eneo la Uhindini Wilaya ya Kilosa ambapo Maleki alichana  'Juzuu Amma' ambacho ni kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislamu.

Amesema alirudishwa mahabusu  katika gereza la Kiberege Wilaya ya Kilombero hadi Februari 20,  2020  kesi hiyo itakapotajwa tena na kwamba upelelezi bado unaendelea.

Jana Maleki alichana kitabu cha dini na picha zake za video kusambaa mitandaoni.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Baada ya kufanya kitendo hicho  Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo alimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kumsimamisha kazi.

Katika video hiyo mtumishi huyo anaonekana akichana karatasi na kuzitupa chini, huku sauti zikisikika za watu wanaomtazama kumuuliza  sababu za kuchana na yeye kujibu: “Nimeamua tu.”

Chanzo: mwananchi.co.tz