Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wapekua nyumba ya Askofu Mwamakula

7988875c769cd84576a59d91c7c1f103 Polisi wapekua nyumba ya Askofu Mwamakula

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepekua nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula.

Juzi Polisi walimkamata askofu huyo, akituhumiwa kuhamasisha maandamano nchi nzima kwa njia ya ujumbe wa maneno katika mitandao ya kijamii. Anatuhumiwa kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi, kuandamana kushinikiza na kudai Katiba mpya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa juzi alibainisha kuwa Jeshi la Polisi kupitia idara ya upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, walimkamata Askofu Mwamakula ili kumhoji.

Mambosasa jana alilieleza HabariLEO kuwa askofu huyo alikamatwa juzi na jana Polisi walikwenda kumpekua nyumbani kwake.

Alisema upekuzi ulifanyika baada ya kumhoji kwa muda mrefu ; na ni sehemu ya utendaji kazi wa jeshi hilo kabla ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Alisema Polisi katika kuhakikisha linatenda kazi zake kwa uwazi, haki na utulivu bila ya kumuonea mtu, lilipopata taarifa za askofu huyo kuhamasisha vurugu, lilimkamata juzi na jana Polisi walimpekua nyumbani kwake.

“Muda siyo mrefu tutakamilisha upelelezi wetu na kisha kuendelea na taratibu kama kawaida za kisheria, nawasihi Watanzania kudumisha amani na ninawapongeza kwa kutoingia barabarani kuandamana,”alisema Kamanda Mambosasa.

Jana gazeti hili liliwasiliana na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Jimbo la Mashariki Kanisa la Moravian Tanzania, Mchungaji Sauli Kajula ambaye alisema hakuna muumini aliyeonesha nia ya kutaka kuandamana.

Chanzo: habarileo.co.tz