Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wanasa mwizi anayetumia hirizi

Tanzania Hirizi aliyokutwa nayo mtuhumiwa

Fri, 15 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Emanuel Hassan mkazi wa Ipogolo kwa tuhuma za kujihusisha na uvunjaji wa nyumba na kuiba kwakutumia funguo bandia  pamoja na hirizi ambayo inadaiwa alikuwa akiitumia wakati wakufanya uhalifu huo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa kamishna msaidizi wa Polisi, Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya msako mkali uliofanywa na jeshi hilo katika kudhibiti matukio ya kihalifu.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani humo linatarajia kuwafikisha mahakamani  watuhumiwa wawili kwa tuhuma za  kukutwa na vipande vinne vya  meno ya Tembo.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live