Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wanaodaiwa kuua kupandishwa kizimbani leo

Napeepic Data Polisi wanaodaiwa kuua kupandishwa kizimbani leo

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis inayowakabili maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara, inatajwa tena leo katika Mahakama ya Wilaya Mtwara.

Washtakiwa wanaohusishwa na mauaji hayo ni ofisa Upelelezi (OC CID) Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara (OCS), Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza na Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Polisi, Marco Mbuta. Wengine ni Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Watuhumiwa hao wanafikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele. Kwa mara ya kwanza, maofisa hao walifikishwa mahakamani hapo Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia.

Siku hiyo, mbele ya Hakimu Kasebele ilidaiwa kuwa Januari 5, maofisa hao wa polisi walimuua Musa Hamis Hamis (25), mkazi wa Nachingwea mkoani Mtwara.

Hata hivyo, hawakupaswa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji na hakimu alisema itaendelea kutajwa hadi upelelezi utakapokamilika na kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Kusini.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz