Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wanamshikilia Mendes, kifo cha mlinzi wake

POLISI WEB Bn Polisi wanamshikilia Mendes, kifo cha mlinzi wake

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Salim Ali, ambaye alikuwa akifanya kazi ya ulinzi katika eneo moja huko Skanska Tegeta jijini Dar es Salaam amefariki dunia na mwili wake kukutwa umetupwa katika eneo la Kibaha Misugusugu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Andros Mendesi ambaye ndiye mmiliki wa eneo hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani

Akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 7, 2022, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema marehemu alikuwa akifanya kazi kwa  Andros Nicodemus Mendesi ambaye kabla ya tukio hilo alifika eneo analofanyia kazi marehemu na kupiga risasi akidai kwamba alikuta wezi kwenye eneo lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live