Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamtambua mvulana aliyefariki ndani ya boksi baada ya miaka 60

Polisi Wamtambua Mvulana Aliyefariki Ndani Ya  Boksi Baada Ya Miaka 60 Polisi wamtambua mvulana aliyefariki ndani ya boksi baada ya miaka 60

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Polisi wamemtambua mvulana aliyepatikana akiwa amefariki ndani ya boksi katika jimbo la Philadelphia zaidi ya miaka 60 iliyopita

Mvulana huyo, aliyefahamika kwa vizazi kama "mvulana ndani ya boksi", ametambuliwa kama Joseph Augustus Zarelli.

Polisi inasema teknolojia ya vinasaba-DNA na kazi ya wachunguzi hatimaye ilisaidia kupata jina la kijana huyo katika kesi ambayo imesalia kuwa ya muda mrefu zaidi ya mauaji ambayo haijapatiwa ufumbuzi.

Usiri kuhusiana na mauji hayo "umeiumiza jamii hii", alisema Kamishna wa polisi wa Philadelphia Police Commissioner Danielle Outlaw.

Katika mkutano wa waandishi wa habari Jumatano, polisi ilisema kuwa hawatatangaza jina la wazazi wa mvulana na wakakataa kusema ni nani aliyehusika na kifo chake.

Kesi hiyo inaendelea kuchunguzwa, polisi inasema, ikiutaka umma kusaidia kuwasilisha maelezo kuhusu maisha ya mvulana huyo.

Polisi walikuwa wamejaribu kutumia kipimo cha vinasaba DNA kutambua utambulisho wa mvulanakwa kutumia mabaki ya mwili wake, lakini sampuli hazikutosha.

Mtaalamu wa uchunguzi wa maiti baadaye aliweza kutumia sampuli za DNA kuwatambua ndugu wa mvulana.

Article share tools

Chanzo: Bbc