Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamsaka aliyetelekeza gari lililopakia bangi

13334 Pic+bangi

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kisarawe. Mtu mmoja  ambaye hajatambulika jina lake  ametelekeza gari lililokutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na kuwakimbia polisi  waliokuwa wakimkimbiza.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 22, 2018 wilayani Kasarawe Mkoa wa Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jonathan Shanna amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, kwamba polisi walilikuta gari hilo likiwa limetelekezwa eneo la shule ya sekondari Minaki, likiwa limepata ajali.

Amesema gari hilo lilikuwa likitokea Gwata Kibaha vijijini kuelekea Dar es Salaam.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafisha bangi kwa maelezo kuwa baada ya upekuzi  katika gari hilo walikuta dawa hizo za kulevya zikiwa katika ndoo tatu za lita kumi na kwenye  gunia.

“Tunamtafuta huyu dereva  maana kitendo cha kuwakimbia polisi pamoja na kukuta bangi katika gari inaashiria kuwa mtu huyu alikuwa mhalifu mzoefu. Pia tumekuta namba za gari zaidi ya moja hii ina maanisha kuwa alitumia njia hiyo kuwakwepa askari,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz