Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamkamata kinara wa wizi wa pikipiki

IMG 20220810 101238 905 Polisi wamkamata kinara wa wizi wa pikipiki

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa maarufu wa wizi wa pikipiki Mkoani Katavi anaefahamika kwa jina la Laurent Lazaro (61) Mkazi wa Kanoge Wilaya ya Mpanda akiwa ameiba pikipiki tano za watu tofauti tofauti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amewaambia wandishi wa Habari ofisini kwake mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo juzi majira ya saa kumi jioni huko katika Mtaa wa Msufini Kata ya Uwanja wa Ndege Manispaa ya Mpanda.

Kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo jeshi la polisi Mkoa wa Katavi waliandaa msako mkali wa kupambana na uhalifu na waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na pikipiki ya wizi yenye Namba za usajiri MC 915 CDV aina ya Honlg yenye rangi nyekundu .

Kamanda Ally Makame alisema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufanyiwa mahojiano ya kina alikiri kuwa aliiba pikipiki nyingine nne kwenye maeneo tofauti tofauti ya Mkoa wa Katavi na aliweza kwenda kuzionyesha pikipiki hiz .

Ambapo katika msako huo walifanikiwa kupata pikipiki hizo nne na kufanya jumla ya pikipiki tano alizokuwa ameiba mtuhumiwa huyo zenye Namba za usajiri MC,445 AAA ina ya SANLG rangi nyekundu , MC 553ADM aina ya SANLG ,MC 468 CUC aina ya SINOREY na MC 802 CQJ aina ya SYNOTEY.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live