Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wamemkamata aliemtoa ujauzito Mariam na kumsababishia kifo

76e317e9d2 Gei 660x400 Polisi wamemkamata aliemtoa ujauzito Mariam na kumsababishia kifo

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, linamshikilia Vestina Michael (44), mkazi wa Buseresere wilayani Chato kwa tuhuma za kumtoa mimba na kumsababisha kifo Mariam Msalaba (40), ambaye alipoteza maisha muda mfupi baada ya kutolewa mimba nyumbani kwa mtuhumiwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Maibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kitendo hicho cha kikatili kimetokea nyumbani kwa mtuhumiwa majira ya usiku.

“Jeshi la Polisi tunamshikilia Vestina Michael, kwamba siku ya Oktoba 31 mwaka huu marehemu alifia nyumbani kwake na ndugu wa marehemu wakaleta malalamiko kwamba, ndugu yao amefia kwa mtuhumiwa wakati akimtoa mimba, hivyo tunamshikilia huyo mtuhumiwa” Kamanda Mwaibambe

Chanzo: millardayo.com