Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waliowaachia huru watuhumiwa ubakaji bibi na mjukuu wake kikaangoni

54807 Pic+ubakaji.png

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga.  Jeshi la polisi mkoani Tanga linawasaka vijana wawili waliokamatwa na kuachiwa wakituhumiwa kuwavamia na kisha kuwabaka mwanamke mwenye umri wa miaka 50 na mjukuu wake wa miaka mitano wakati wakitoka shambani.

Mbali na kusakwa kwa watuhumiwa hao, askari waliohusika kuwaachia huru watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Aprili 30 kuhusu kuachiwa huru kwa watuhumiwa hao, kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema Aprili 18 mwaka huu saa 10:00 jioni katika vichaka vya  kijiji cha Jaributena, mwanamke huyo akiwa na mjukuu wake wa miaka mitano walivamiwa na kubakwa na vijana aliodai walipokezana kufanya kitendo hicho kiovu.

“Nimeamua kusimamia mwenyewe tukio hili, tutachunguza upya na kuwakamata waliotuhumiwa lakini askari wa kituo cha Pongwe waliowakamata na kuwaachia  huru tutawashughulikia kwa mujibu wa taratibu zetu,” amesema Kamanda Bukombe.

Amesema atahakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na jalada lao kufikishwa kwa mwendesha mashtaka wa Serikali ili mchakato wa kuwafikisha mahakamani ufanyike haraka.

Mtoto wa mwanamke aliyefanyiwa ukatili huo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, amesema wawili hao walikuwa wakitoka kitongoji cha Jaributena kuelekea Pongwe ambako njiani walifuatwa na vijana wawili waliowavamia na kuwapeleka vichakani.

Amesema baada ya udhalilishaji huo, mwanaye alipelekwa hospitali kwa matibabu na kuomba vyombo mbalimbali vya utetezi wa haki za binadamu kuingilia kati.



Chanzo: mwananchi.co.tz