Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wakuna kichwa ubakaji, mauaji ya wanawake Tanga

29976 Ubakaji+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Wanawake wawili wamebakwa mkoani Tanga ndani ya  saa 72 na kisha kuuawa, jambo ambalo Kamanda wa Polisi mkoani humo, Edward Bukombe amesema ni lazima wabaini  kiini cha wanaobakwa kuuawa.

Matukio hayo ya kusikitisha yametokea wilayani Pangani na jijini Tanga ambako usiku wa Desemba Mosi, 2018 mwanamke mmoja alikutwa amekufa kwa kunyongwa baada ya kufanyiwa udhalilishaji huo.

Leo alfajiri Desemba 3, 2018, mwanamke mwingine mwili wake ulikutwa kichakani katika kitongoji cha Mwakizaro, Kata ya Mwanzange ukiwa na jeraha kichwani.

Miezi miwili iliyopita wanawake wawili waliuawa mkoani humo baada ya kubakwa.

Akizungumza na Mwananchi leo, Bukombe amesema, “matukio haya yametupa kazi ya ziada  kuchunguza. Ni kwa nini vijana wanawaingilia kimwili wanawake na kisha kuwaua. Ni tamaa gani hizi za ngono?”

Amesema hadi leo saa 9 alasiri polisi walikuwa wanawashikilia watu wawili wakazi wa Bweni wilayani Pangani wakihusishwa na mauaji hayo.

“Kijana mmoja alikamatwa kijiji cha Sakura kilichopo kilomita 57 kutoka eneo la tukio akijaribu kutoroka kwa kutembea kwa miguu. Katika mahojiano ya awali alikiri kuhusika na tukio hilo lakini vyombo vya sheria ndivyo vitakavyomtia hatiani,” amesema Bukombe.

Amemtaja mwingine anayeshikiliwa akihusishwa na mauaji ya mwanamke mwingine kuwa alikamatwa usiku wa kuamkia leo na walinzi wa jadi maarufu kwa jina la Sungusungu.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz