Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wakamata dhahabu ya Bil. 9 iliyokuwa ikitoroshwa

Polisi Wakamata Dhahabu Ya Bil. 9 Iliyokuwa Ikitoroshwa Polisi wakamata dhahabu ya Bil. 9 iliyokuwa ikitoroshwa

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limekamata mawe ya dhahabu yenye uzito wa gramu 6753.4, yenye thamani ya shilingi bilioni tisa, yakitoroshwa kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama sambamba na Carbon yenye madini yadhaniwayo kuwa ni dhahabu yenye uzito wa kilogram 261 ambayo thamani yake bado haijafahamika.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, ACP Janeth Magomi amesema mali hizo zimekamatwa eneo la Manzese Manispaa ya Shinyanga, ambapo zimekamatwa kwa kipindi cha kuanzia tarehe 26/07/2023 hadi tarehe 22/08/2023 baada ya kufanya misako na doria katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Amesema, katika misako hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata Bunduki aina ya Rifle yenye namba 2/49PF78701 ambayo ilikuwa inatumika katika shughuli za ulinzi bila kibali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live