Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waingilia kati ishu ya Teleza "Tumemkamata Alfajiri" (Video+)

Video Archive
Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema limemkamata Mtu ambaye jina lake limehifadhiwa lakini mazingira waliyomkamata Mtu huyo ni katika mazingira ya kutatanisha baada ya Wananchi kukaa kikao katika kata ya Murieti kulalamika kusumbuliwa na Mtu waliyempa jina la Teleza kwasababu ya kutembea na mafuta na kubaka akina Mama.

“Mnamo mwezi wa nane mwaka huu majira ya saa sita za mchana katika maeneo ya murumbo kulifanyika Ulinzi na Usalama katika maeneo hayo ambapo vilihusisha zVikundi vya Ulinzi shiriki na katika kikao hicho kulijitokeza taarifa za kuwepo kwa mtu ambae anaingia katika Nyumba za Watu nyakati za Usiku”– Polisi Aruasha

“Baada ya kupata taarifa hizi Jeshi la Polisi lilianza Uchunguzi wakina kwa ushirikiano wa Wananchi na pamoja na timu ya Makechero ambapo Alfajiri Agosti 10, 2021 huko maeneo ya Murumbo tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja jina tumelihifadhi na Uchunguzi unaendelea“- Polisi Arusha

“Nitoe wito kwa Wananchi na Vyombo vya Habari za uhalifu na wahalifu ili tuendelee kukomesha uhalifu katika Mkoa wetu”- Polisi Arusha

Chanzo: millardayo.com