Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi wafafanua madai ya kumteka raia Songwe

Msemaji Jeshi La Polisi Polisi wafafanua madai ya kumteka raia Songwe

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikielekeza kuwa Joshua Mkandi wa mkoani Songwe ametekwa na Jeshi la Polisi na hajulikani alipo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, Joshua Mkandi alikamatwa na Askari na Polisi waliojitambulisha kwake wakiwa wamevaa sare za Polisi, hata aliyeandika taarifa ya uposhaji kwa umma anaeleza hivyo.

Wamesema, ifahamike Mkandi alikamatwa pamoja na wenzake 12 wakituhumiwa kwa makossa ya unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi wa pikipiki na kufikishwa kituoni kwa mahojiano kisha watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Jeshi la Pilisi limesema halitarudishwa nyuma kwa taarifa zozote zile za upotoshaji ambazo malengo na nia yake haijulikani, badala yake litaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda maisha ya watu na mali zao kwa msingi ya sharia, haki, kanuni na taratibu zilizopo.

Aidha, jeshi la Polisi limetoa onyo kwa wale wenye tabia za kutumia kurasa zao kwa kuandika taarifa za upotoshaji na uzushi ambazo malengo yake wanayajua wao na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live