Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waendelea kumshikilia Zitto

25059 Zitttto+pic TanzaniaWeb

Fri, 2 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kumshikilia kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo,  Zitto Kabwe.

Leo mchana Alhamisi Novemba Mosi, 2018, Zitto amerudishwa kituo cha polisi Mburahati  akitolewa kituo cha polisi Oysterbay alikopelekwa tangu asubuhi.

Zitto alikamatwa na polisi jana saa  3 asubuhi nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa tatu kituo cha  Oysterbay na baadaye kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi, jioni kupelekwa Mburahati.

Akizungumza na Mwananchi  wakili wa mwanasiasa huyo, Jebra Kambole amesema  Zitto amerudishwa katika kituo cha Mburahati.

"Hadi sasa bado mteja wangu hajapatiwa dhamana na polisi lakini tayari nimeshawasilisha maombi mahakamani ya kutaka apewe dhamana ila tumechelewa tunaamini kesho yataanza kufanyiwa kazi," amesema Kambole.

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu amesema hadi sasa kiongozi wake hajapewa dhamana badala yake anazungushwa kila kona.

“Hatuna jinsi tunafuata polisi wanavyotaka maana sasa hivi kiongozi wangu amerudishwa Mburahati," amesema Ado .

Zitto alikamatwa na polisi siku moja baada ya Polisi mkoani Kigoma kumtaka awasilishe vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018 kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika tukio la mapigano ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya Uvinza mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amesema tuhuma za mbunge huyo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.

Polisi wafanya upekuzi nyumbani kwa Zitto

Zitto ahamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi

Zitto Kabwe alivyonaswa na polisi Dar

Chanzo: mwananchi.co.tz