Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waendelea kumng’ang’ania Halima Mdee

66868 Pic+mdee

Mon, 15 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Polisi mkoani Kagera nchini Tanzania linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa chama kikuu cha upinzani nchini humo (Bawacha), Halima Mdee.

Polisi walimkamata Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema) jana jioni Jumapili Julai 14m, 2019 mara baada ya kumaliza kikoa cha ndani cha wanawake kilichofanyika Bukoka mjini mkoani humo huku wengine wakiachiwa kwa dhamana.

Mwenyekiti wa Bawacha mkoani Kagera ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Conchesta Rwamulaza akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15, 2019 amesema Mdee amekamatwa kwa sababu ambazo hazijatajwa.

Amesema kikao chao kilikuwa cha ndani na yeye alikuwa miongoni mwa waliohojiwa jana Jumapili kituo cha polisi Bukoba na kuachiwa.

Amesema kikao hicho kilihusu uchaguzi wa Bawacha Manispaa ya Bukoba na Mdee alikuwa ni miongoni mwa viongozi walioalikwa ambapo aliambatana na Katibu wa Baraza hilo, Grace Tendega.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha jana wamekusanyika kwa makundi nje ya kituo cha Polisi Bukoba wakifuatilia hatima ya dhamana ya Mbunge huyo.

Pia Soma

Jitihada za Mwananchi kumpata kamanda wa Polisi mkoani humo hazijazaa  matunda kwani ofisini kwake hayupo wala simu zake za mkononi hazipokelewi.

Chanzo: mwananchi.co.tz