Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi waeleza mtuhumiwa alivyombaka binti wa miaka sita

40005 Pic+ubakaji Polisi waeleza mtuhumiwa alivyombaka binti wa miaka sita

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Polisi mkoani Tabora wanamshikilia mkazi wa kitongoji cha Utemini kata ya Ushokola wilayani Kaliua, Amos Zakaria kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka sita.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 4, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea jana saa sita mchana.

Amesema mtuhumiwa alimvizia binti huyo wakati anapita na kumvutia bafuni kisha kumbaka.

Amesema polisi walimkamata na baada ya kukamilisha maelezo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.



Chanzo: mwananchi.co.tz