Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kuwakamata Wanaume wanaowanunua dada poa

Vyangudiii Kamanda Muliro amesema wameamua kuja kivingine bila kutumia nguvu

Tue, 5 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa sehemu ya mikakati yake katika kuzuia biashara ya wanawake kujiuza ni kuwakamata wanaume ambao wanahusika katika biashara hiyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema ameamua kuja na staili tofauti ambayo haitahusisha matumizi ya nguvu kwa wanawake wanaofanya biashara hiyo.

“Kuna sehemu tuliweka kambi kwa siku tatu, hatukuwakamata wanawake amBao walikaa pale wakipigwa na baridi kwa siku zote hizo, wanaume hawakutokea na ndiyo tuliokuwa tukiwasubiri, baada ya kuona hakuna wateja wanawake hao hawakurudi eneo hilo.

“Nimeelekeza na kuagiza wanaume wakamatwe kwa kuwa kama hawataenda maeneo hayo basi hiyo biashara haitakuwepo,” - Muliro

Chanzo: www.tanzaniaweb.live