Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kuongoza msako wa wezi wa umeme, maji Dar

12488 Pic+mambo+sasa TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) wametoa siku saba kwa wezi wa maji na umeme kujisalimisha.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Agosti 17, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amebainisha kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la watu kujiunganishia maji na umeme bila kufuata utaratibu na kusababisha kampuni hizo kupata hasara.

 

“Kuanzia Agosti 27 tutaanza msako mkali kwa watu hawa ili tuweze kuwabaini,” amesema Mambosasa.

Kwa upande wake ofisa mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema hakuna haja ya watu kuiba maji kwa kuwa shirika hilo lina huduma ya kuunganisha maji kwa mkopo.

“Kwa sasa shirika letu lina maji ya kutosha na tunayo huduma ya kusambaza maji kwa mkopo, hakuna sababu ya watu kuiba maji,” amesema.

Meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amesema watashirikiana na polisi kuhakikisha wezi wanadhibitiwa, wakiwemo wanaoiba mafuta ta transfoma.

“Tutashirikiana na polisi kuhakikisha wote wanaohujumu miundombinu hii tunawakamata kwa kuwa wamekuwa wakilitia hasara shirika hasara kwa kuiba mafuta,” amesema Leila.

Katika kuweka msisitizo, Mambosasa amesema wote watakaokaidi kujisalimisha katika vituo vya polisi, watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Chanzo: mwananchi.co.tz