Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kukusanya taarifa za ajali kidigitali

Polisi Digital Polisi kukusanya taarifa za ajali kidigitali

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Wakati ajali za barabarani zikiendelea kuwa tatizo sugu nchini, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imewezesha utengenezwaji wa programu ya kurekodi taarifa za ajali kwa njia ya mtandao na kuikabidhi kwa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa takwimu za ajali.

Programu hiyo iliyobuniwa na kampuni ya Smart Code itaanza kutumika jijini Dar es Salaam kwa majaribio ya miaka miwili kabla ya kuongezwa hadi mikoa mingine ambapo askari wa usalama barabarani wataweza kukusanya taarifa za ajali kupitia programu hiyo ambayo inapatikana kwenye simu janja.

Akizungumza wakati wa kukabidhi programu hiyo ya usalama leo Novemba 30 jijini hapa, Ofisa Masoko wa Smart Codes, Johnson Bebwa amesema ndani ya dakika nne askari atakusanya na taarifa zote katika eneo la tukio na kuzituma kunakohusika bila kumlazimu yeye kufunga safari kama inavyofanyika sasa.

Amesema kwa teknolojia hiyo mpya, askari wa usalama barabarani wataweza kukusanya taarifa za ajali katika eneo la tukio, kujaza kwenye programu ya usalama na kuziwasilisha Makao Makuu ndani ya dakika tatu hadi nne.

Bebwa ameelza kuwa mfumo uliopo sasa askari wanalazimika kutumia muda mwingi kukusanya taarifa za ajali na kuzipeleka makao makuu wakati kupitia programu hiyo taarifa zitakusanywa na kutumwa kielektroniki.

"Sahau kuhusu muda ambao trafiki wa polisi alitumia kwenda kwenye eneo la tukio, kukusanya data na kurudi ofisini. Baada ya kurejea ofisini, huwachukua hadi dakika 10 kuandaa ripoti,” amesema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa usambazaji wa TBL, Nancy Riwa amesema kampuni hiyo imegususwa kuwa sehemu ya kupambana na ajali za barabarani zinazogharimu maisha ya watanzania wengi.

“TBL inajivunia kuzinduliwa kwa App ya Usalama Barabarani, hii ni hatua nyingine tuliyoichukua ili kuboresha usalama nchini Tanzania kwa kuzingatia ukweli kwamba usalama barabarani ni muhimu kwa takribani nyanja zote za maisha ya kila siku na ni muhimu katika kujenga miji na jamii endelevu.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Ramadhani Ng’anzi akizungumza katika uzinduzi huo, mesema uwepo wa programu hiyo utalisaidia jeshi la polisi kukusanya tkwimu za uhakika zinazohusu ajali na kuweza kutambua ni kundi gani gani linaathirika zaidi.

Amesema Jeshi la Polisi litatoa kila aina ya ushirikiano utakaohitajika katika kipindi cha majaribio ya matumizi ya programu hiyo ili matokeo yake yapatikane kwa haraka na ikiwezekane ianze kutumika nchi nzima.

"Takwimu ni kioo cha taasisi, kupitia programu hii tutaweza kujua tunaendaje katika utendaji wetu, je ajali zinaongezeka au zinapungu, kundi gani linaathirika zaidi. Kikosi sasa kinaenda kuondokana na mambo ya makaratasi tunakwenda kukusanya taarifa kidijitali,” amesema.

Chanzo: Mwananchi