Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kuja na mkakati huu kuimarisha ulinzi

MULIRO 1 Kamanda Jumanne Muliro

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Jiji la Dar es Salaam likielezwa kuwa na changamoto ya uhalifu, Jeshi la Polisi limesema kila mwananchi ana jukumu la kulinda usalama katika eneo lake.

Hayo amewekwa wazi na Kmand wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro na kuongeza kusema kuwa kwa ukubwa wa Jiji hilo ni ngumu kwaaskari kuwea kufika kila maeneo.

Muliro amesisistiza kuwa kutokana na changamoto ya ukubwa wa jiji hilo wao kama jeshi la ulinzi wanautaratibu wa kutimiza majukumu yao sambamba na kuwafikia wanannchi wote ka ukaribu.

Muliro: Kwanza polisi tunataka tutoke huko kwamba polisi wawepo popote. Kitu tunachotaka watu wafuate sheria, suala sio kujaza polisi.

Sio kila unapokwenda uone polisi, ni dalili mbaya za nchi, watu wake kutofuata sheria, wala sio dalili nzuri kwa polisi kwamba wamefanya kazi kubwa.

Hata wale tunaowakalisha muda wa kazi mwingi tunaangalia muda gani kuna magari mengi ni mchana, usiku yanapungua, vinginevyo tutasema polisi walale barabarani, ambao ni mtazamo mchafu kabisa.Tunataka watu wafuate sheria ili polisi wapungue barabarani.

Nenda kaangalie Sheria ya Serikali za Mitaa, inakwambia, Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa ndio mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mtaa ule.

Maana yake wewe ni mtu mkubwa, unaratibu masuala ya kuzuia vitendo vya kihalifiu, matishio ya usalama kwenye eneo lako. Ukiratibu vizuri Polisi Kata anakuletea timu mara moja, unamaliza kazi yako. Mitaa inayofuata mifumo wa usalama chini ya mifumo ya Serikali za Mitaa, wahalifu hawataingia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live