Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kuimarisha ulinzi maonyesho ya Sabasaba

64682 POLIS+PIC

Fri, 28 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati leo Ijumaa  Juni 28,2019 maonyesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yakianza tarajiwa kuanza ramsi, Kamanda wa Polisi wa mkoa  wa Kipolisi Temeke, Amon Kakwale amesema  jeshi hilo limechukua hatua zote kudhibiti vitendo vya uhalifu kwenye maonyesho hayo.

Kamanda Kakwale ameyasema hayo jana Alhamisi Juni 27, 2019 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu polisi kuimarisha ulinzi na usalama wakati wote wa maonyesho ya Sabasaba  yanayofanyika wilayani Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania.

“ Watanzania na wageni kutoka nchi mbalimbali waje kutembelea wasihofie jambo lolote, tumeimarisha ulinzi kwenye maonyesho haya ya makubwa nchini. Waje na watembee kifua mbele wasiogope chochote,” amesema Kamanda Kakwale.

Amesema kunapokuwa na mkusanyiko wa watu wengi, vibaka na wahalifu hutumia nafasi hiyo kutekeleza uhalifu, lakini katika maonyesho hayo hawatapata nafasi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz