Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi kuchunguza mauaji ya Padre Mbeya

Batch Kanisa Parokia Galula88 Polisi kuchunguza mauaji ya Padre Mbeya

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkonai Mbeya limethibitisha kutokea mauaji ya Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya wa Shiriki wa Wasionari wa Afrika (White Father), Michael Samson huku likieleza kuendelea na uchunguzi kujua chanzo cha kifo hicho.

Padre Samson anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa viungo na kutengenishwa kisha kutupwa katika mto Meta maeneo ya Sabasaba jijini hapo.

Katika taarifa iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Mbeya, Mhashamu Gervas Nyaisonga jana Jumamosi ilieleza kuwa Padre Samson alitoweka Juni 10 katika kituo cha Vijana kanisa Katoliki Mbeya saa 12 jioni.

Taarifa hiyo ilieza kuwa baadaye mwili wa padre huyo uliokotwa maeneo ya Sabasaba jijini humo Juni 11 majita ya saa 4 asubuhi.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya (RPC), Ulrich Matei amesema wanaendelea kufanya uchunguzi kunaini chanzo cha mauaji hayo, kwani marehemu alikuwa raia wa Malawi na kuwaomba wananchi kutoa taarifa ili kukamatwa kwa wahusika.

Amesema kwa uchunguzi wa awali wamebaini ni mauaji ya makusudi na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kutumia njia za kisayansi ili kumbaini aliyetekeleza mauaji hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live